Rais wa Jamhuri ya Poland Mheshimiwa Andrzej Duda ameondoka nchini usiku huu na kuagwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb). Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijiji Dar es Salaam, baada ya kuhitimisha ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili hapa nchini.
Akiwa Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Rais Duda ambaye aliambatana na Mke wake, Bi. Agata Korhauser-Duda, aliangalia burudani ya ngoma kabla ya kupanda ndege yake maalum, na kuanza safari ya kurejea nchini Poland.
Katika tukio hilo la kuaga, Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Kale na Utalii-Zanzibar, Mhe. Mudrick Soragha na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo.