Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameongoza kikao cha majadiliano na Ujumbe kutoka Wizara ya Madini ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Anthony Mavunde, kuhusu namna Sekta ya Madini inavyoweza kuongeza mchango wake katika kukuza pato la Taifa.
Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Bw. Kheri Mahimbali, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, na Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Shirika la Madini (STAMICO), na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).