Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameshiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Chuo cha Biashara Tanzania (CBE) pamoja na uzinduzi wa Dira ya Miaka 50 ijayo ya Chuo hicho, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha vyuo vyake mbalimbali nchini, ikiwa ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuhakikisha sekta ya elimu ikiwemo elimu ya biashara inakuwa na mchango mkubwa katika kukuza ajira, uwekezaji na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Maadhimisho hayo yaliongozwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb), ambaye Wizara yake inakisimamia Chuo hicho, Bodi ya Wakurugenzi, Uongozi wa Chuo, Wanafunzi, Viongozi wastaafu waliofanya kazi katika Chuo hicho kwa nyakati tofauti ambao walipewa tuzo pamoja na wadau wengine mbalimbali.

Share Story