Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), akitoa hotuba yake fupi katika hafla ya utoaji tuzo kwa walipakodi waliofanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2023/24, ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miongozo anayoitoa katika ukusanyaji wa Kodi bila kutumia mabavu.

Amesema kauli ya Mhe. Rais kutaka Kodi ikusanywe kwa hiari imezaa matunda kwa kupatikana kwa makusanyo makubwa ya Kodi, pia Mhe. Rais ameunda Tume ya kufanya mapitio ya Sheria za Kodi na kuiwezesha TRA kujenga mifumo inayoweza kuleta tija kwenye makusanyo.

Dkt. Mwigulu amesema katika kipindi hiki cha Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kiasi kikubwa fedha katika sekta ya Kilimo, huduma za jamii, sekta ya Afya na katika Miundombinu ambapo barabara zinajengwa mijini na vijijini.

Share Story