Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea taarifa ya maandalizi ya tukio la utoaji tuzo kwa wafanyabiashara katika kilele cha Siku ya Mlipa Kodi, kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda, hafla inayotarajiwa kufanyika leo usiku tarehe 23 Januari 2025 katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha na viongozi wengine wa Wizara ya Fedha na TRA.