Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb), katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwapokea wageni mbalimbali akiwemo Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinwumi Adesina, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia masuala ya Utawala, Bi, Anna Bjerde, wanaotarajiwa kuwasili nchini usiku wa leo kwa ajili ya kushiriki Kilele cha Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi za Afrika, utakaofanyika kuanzia tarehe 27-28 Januari, 2025, Jijini Dar es Salaam.
