Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameshiriki hafla ya kuzindua mkopo maalumu wa Benki ya NMB, wa kuwakopesha wafanyabiashara wadogo na wa kati wa biashara ya nishati safi, shilingi za Kitanzania bilioni 100, katika kipindi cha miaka miwili, mahsusi kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa miradi, na biashara zinazolenga kupeleka Nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.
Akitoa salaam zake katika hafka hiyo iliuotanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, na kuongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko, Mhe. Dkt. Nchemba aliipongeza NMB, kwa kutekeleza maono ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anayeimamia kwa dhati agenda ya kitaifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuhifadhi mazingira, kulinda afya za watu na kuimarisha uchumi wa nchi.