Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amezindua Kitabu kiitwacho “The Magnets of Good Fortunes: A concise Guide to Success”, kilichoandikwa na Dkt. Dr. Mosses Mwizarubi, ambaye ni Msaidizi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam, ambapo alimpongeza Mwandishi wa Kitabu hicho kinachogusa maeneo mbalimbali ya maisha na kuhamasisha ustawi wa maisha na mafanikio kwa kumiliki mali, na kutoa rai kwa Jamii kujenga utamaduni wa kusoma na kuandika vitabu kwakuwa ni nguzo muhimu ya maendeleo na ustawi wa jamii yoyote ile duniani.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri, akiwemo Gavana wa Benki ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Manaibu Gavana, Bi. Sauda Mwema na Dkt. Yamungu Kayandabila, Wazazi wa Dkt. Moses Mwizarubi pamoja na mke wake, Wakuu wa Taasisi za Fedha, Uongozi Institute na wanazuoni mbalimbali.