Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina, na Mkurugenzi Mtendaji wa Utawala wa Banki ya Dunia, Bi. Anna Bjerde, wamewasili nchini leo usiku tarehe 25 Januari 2025, Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamepokelewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi utawakutanisha Wakuu wa Nchi za Afrika na wadau muhimu wa sekta ya nishati ili kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
Mkutano huo inatarajiwa kuwa utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 inafanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kufukia 35.