Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amehutubia wakati wa Mjadala kuhusu mchango wa Washiriika wa Maendeleo wa Kimataifa, katika kuchangia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa nishati ya uhakika, kuelekea Kilele cha Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaotarajiwa kufanyika kesho (28.01.2025), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo ametoa wito wa nchi za Afrika kwa kushirikiana na Taasisi za fedha za Kimataifa na Sekta binafsi kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha Sekta ya nishati Barani Afrika itakayochangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa maendeleo endelevu yatakayosaidia kukuza ajira, uchumi endelevu na kuboresha maisha ya watu.

Share Story