Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Nchi Wizara ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani, Mhe. Jochen Flasbarth, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo yao, walikubaliana kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Serikali ya Shirikisho la Ujerumani.
Kikao hicho kiliwashirikisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Khamis Shaaban na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani.