Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund for Arab Economic Development), Bw. Albahar Waleed, Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo yao, walikubaliana kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na Mfuko huo kupitia ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za maji, umaendeleo ya miundombinu, na huduma jumuishi za kijamii.

Kikao hicho kiliwashirikisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Khamis Shaaban, Mkuu wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika, Mhe. Balozi Abdalah Kilima, Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait.

Share Story