Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu (Asian Infrastructure Investment Bank – AIIB), Bw. Jin Luqun, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza leo (27.01.2025), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana namna ya kuendeleza ushirikiano wa katika kuboresha miundombinu nchini, ukiwemo Mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa (SGR).

Kikao hicho kiliwashirikisha pia Kamishna Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Benki hiyo.

Share Story