Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Ibrahim Mohamed Abdourazak, Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, uliohitimishwa tarehe 28 Januari 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili namna ya kuongeza ushirikiano kupitia biashara na uwekezaji.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha wa Comoro, Mhe. Ibrahim Mohamed Abdourazak, alisema kuwa nchi yake inajivunia uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili na kumwomba Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Nchemba kuzihamasisha Taasisi za Fedha za Tanzania kufungua huduma zao nchini Comoro ili kurahisisha biashara na uwekezaji ili kukuza uchumi, kwa faida ya nchi hizo mbili.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Said Yacoub, Kamishna wa Idara ya Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha ya Comoro.