Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Libya, Mhe. Dkt. Khalid Al Mabrouk Abdalla, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi na Serikali, uliohitimishwa tarehe 28 Januari 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadili namna ya kuongeza ushirikiano kupitia Sekta mbalimbali za uzalishaji.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Kamishna wa Idara ya Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule, na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha ya Libya.