Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, wakati wa Kongamano la Tatu la Kahawa Barani Afrika, lililofungwa rasmi leo na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam-JNICC, ambapo msisitizo mkubwa kwa nchi 25 za Afrika zinazozalisha kahawa ni kuongeza thamani ya zao hilo ili kuongeza mnyororo wa thamani ili liweze kuchangia zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi hizo pamoja na kukuza ajira hususan kundi la vijana.

Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa Nchi za Afrika kwa pamoja zinapata wastani wa dola bilioni 2.5 kila mwaka kutokana na mauzo ya kahawa nje ya nchi wakati biashara ya kahawa duniani ina thamani ya dola bilioni 500, mapato hayo madogo ni kutokana na kuwa zaidi ya asilimia 90 ya kahawa ya Afrika inasafirishwa kama malighafi.

Share Story