Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), akiwa katika Treni ya Kisasa (SGR) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Belete Nathan na abiria wengine kutoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma. Mradi wa SGR ambao kipande cha kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma kimekamikika, ni miongoni mwa miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Serikali na umepata uungwaji mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia na umekuwa Mradi maarufu unaotumiwa na watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali.
youtu.be/NYud6aIZPfY