Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefungua Mhadhara wa 9 wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Marehemu Gilman Rutihinda (1988-1993), uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro, Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, uliobeba kaulimbiu ya “Kuongoza Mageuzi ya Uchumi wa Kidigitali: Fursa za Ubunifu wa Kifedha na Ujumuishaji”, ambapo Dkt. Nchemba, alitoa wito kwa watanzania kufanya miamala kwa njia za kidigitali badala ya kutumia fedha taslimu kwa kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika mifumo ya kidigitali inayowezesha kufanya matumizi kwa njia hizo kupitia mitandao ya simu, benki na njia nyingine.

Mhadhara huo, umehudhuriwa na familia ya Marehemu Rutihinda, ikiongozwa na Mjane wa Marehemu, Bi. Josephine Rutihinda, pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi na fedha kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Gavana Gilman Rutihinda, aliyefariki dunia akiwa madarakani mnamo mwaka 1993 baada ya kufanya mageuzi makubwa katika sera za uchumi na fedha kwa kuhimiza ubunifu na matumizi ya kidigitali katika kuendesha uchumi wa nchi.

Share Story