Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2024/25 ya shilingi trilioni 50.29.
Hafla hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.