Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wamewasilisha Mapendekezo ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka wa Fedha 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka wa Fedha 2024/25 ya shilingi trilionin 50.29.