Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Uwakilishi kutoka Shirika la Kikanda la Umoja wa Mataifa lijulikanalo kama United Nations African Institute for the Prevention of Crime and the Treatment of Offenders (UNAFRI), lenye Makao Makuu yake Kampala, Uganda, ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi wake Mkuu, Bw. Munanura Andrew Karokora, kando ya Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), ambapo walijadili masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Taasisi hiyo katika wajibu wa kifedha (financial obligations).

Pamoja na hayo, walijadili pia uwezekano wa ushirikiano wa UNAFRI na Wizara katika kuratibu programu za mafunzo na tafiti kwa taasisi za Wizara pamoja na taasisi nyingine za kifedha hususani katika masuala ya uzuiaji uhalifu wa kifedha (financial crime prevention).

Kikao hicho kifupi kiliwashirikisha pia Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na Dkt. Ahmed Linga ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Programu wa UNAFRI.

Share Story