Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Uchukuzi wa Uganda, Jenerali Edward Katumba Wamala, Kando ya Mkutano wa 50 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), jijini Kampala-Uganda, ambapo wamejadiliana kuhusu namna Reli ya Kisasa ya SGR, inaweza kusisimua biashara kati ya nchi hizo mbili kwa kutumia Kituo cha Mwanza ambapo mpango uliopo ni kuifanya mizigo inayotoka Bandari ya Dar es Salaam kuelekea Uganda, ivushwe kwa njia ya vivuko maalum kupitia Ziwa Victoria.
Dkt. Nchemba alisema kuwa Mradi huo wa SGR umefikia zaidi ya asilimia 60 na kushauri Mamlaka za Tanzania na Uganda kupitia Timu za Wataalamu zianze kufikiria kutumia fursa hiyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo kati ya nchi hizo mbili, pendekezo ambalo liliungwa mkono na Jenerali Edward Katumba Wamalwa.
Katika kikao hicho, Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Simuli na Kamishna wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja.