Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amepata mapokezi makubwa ya Viongozi, wanasiasa na wakazi wa Tunduma na vitongoji vyake alipofika kuwa Mgeni Rasmi na kushuhudia utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tunduma,- Vwawa, uliofanywa na Wizara ya Maji, utakaogharimu shilingi bilioni 119.9 za Tanzania, kutoka chanzo cha maji ya Mto Momba, ulioko Wilayani Momba, mkoani Songwe.
Mradi huo unatarajia kuwanufaisha wakazi 219,309 katika Miji ya Tunduma, Vwawa na Mlowo, ambapo ujenzi wake utachukua miezi 18 kukamilika na kuanza kutoa maji safi na salama kwa wananchi.