Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameshiriki hafla ya Ufunguzi wa Kikao cha ngazi ya Juu cha Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Fedha Haramu (The Financial Action Task Force (FATF) Africa Joint Group), kikao kilichofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akimkaribisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhutubia, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa Tanzania imeweka mifumo madhubuti ya kukabiliana na vitendo vya utakasishaji fedha haramu na udhibiti wa vitendo vya ufadhili wa ugaidi na kwamba iko tayari kushirikiana na Kikosi kazi hicho kinachoongozwa na Bi. Yonesha Sahye, ambacho kiko nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya nchi ilivyojipanga kukabiliana na vitendo hivyo vya utakasishaji fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na udhibiti wa usambazaji wa silaha za maangamizi kwa viwango vya kimataifa.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mh. Dkt. Saada Mkuya Salum, Mh. Innocent Bashungwa [Waziri wa Mambo ya Ndani – JMT], Mh. Dkt. Doroth Gwajima [Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum], Eng. Zena Said [Katibu Mkuu Kiongozi – SMZ], Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Bw. Eliakim Chacha Maswi (Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria), Bw. Emmanuel Tutuba [Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania], Bi. Sauda Msemo [Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Wataalamu Mbalimbali dhidi ya Utakatishaji Fedha Haramu] na Bw. Majaba Magana [Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu] na Viongozi wengine wa Serikali.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *