Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewasili Washington D.C nchini Marekani, ambako anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Msimu wa Kipupwe ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, ambayo Mwaka huu 2025, imebeba kaulimbiu ya “Ajira: Njia ya Mafanikio”.

Katika msafara huo, Mhe. Dkt. Nchemba ambaye ni Gavana wa Benki ya Dunia, ameambatana na Magavana wasaidizi wa Benki hiyo, ambao ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.

Viongozi wengine ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu wa Baraza la Mawaziri, Bw. Nsubili Joshua, Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Masuala ya Uchumi, Dkt. Blandina Kilama na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Ujumbe wa Tanzania, umekaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza na kufuatiwa na kikao cha maandalizi kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania mjini Washington D.C ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Balozi Kanza alitoa taarifa ya utendaji kazi wa Ubalozi huo, iliyoonesha mafanikio makubwa katika kukuza biashara na diplomasia ya kiuchumi kati ya Tanzania na Marekani.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *