Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), kushoto, akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Akwinumi Adesina, walipokuta katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Abidjan, Côte d’Ivoire, mahali ambapo unafanyika Mkutano Mkuu wa mwaka 2025, ambao utakuwa wa 60 wa Bodi ya Magavana wa AfDB na wa 51 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), ulioanza jana tarehe 26 hadi 30 Mei 2025, na utajumuisha uchaguzi wa Rais mpya wa Benki hiyo atakayemrithi Dkt. Adesina ambaye ni raia wa Nigeria na pia utafanyika uchaguzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi hiyo kubwa ya fedha barani Afrika.
Zaidi ya wajumbe 6,000 wanatarajiwa kuhudhuria, wakiwemo Marais na Wakuu wa Serikali za Afrika, Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Mabenki Kuu, washirika wa maendeleo, wawakilishi wa sekta binafsi, viongozi wa asasi za kiraia, wasomi, taasisi za utafiti, NGOs, na wadau wengine. Ukiwa na Kaulimbiu “Kufanya Rasilimali za Afrika Kufanya Kazi kwa Maendeleo ya Afrika”.
Mhe. Dkt. Nchemba anamtaja Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB anayemaliza mhula wake, Dkt. Akwinumi Adesina, kuwa ni kiongozi mahili na mtu muhimu katika maendeleo ya Tanzania tangu alipochukua uongozi wa Taasisi hiyo ambapo kupitia ufadhili wa miradi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Tanzania imepiga hatua kubwa kimaendeleo.