Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake Dkt. Akinumwi Adesina, kando ya Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire Jijini Abidjan nchini Côte D’ivoire, ambapo pia Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), alishiriki Mkutano huo akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Côte D’ivoire, mwenye Makazi yake nchini Nigeria Balozi Selestine Kakele, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Taasisi hiyo ya Fedha.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *