Waziri wa Fedha wa Tanzania, ambaye pia ni Gavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Gavana Mbadala (alternating Governor) wa Benki hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakifuatilia matukio mbalimbali baada ya Bodi ya Magavana ya Benki hiyo kumchagua kwa kura nyingi, Dkt. Sidi Quld Tah (Raia wa Mauritania), kuwa Rais Mteule mpya wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), katika uchaguzi uliofanyika leo tarehe 29 Mei 2025, katika Hoteli ya Sofitel Ivoire, Jijini Abidjan nchini Côte D’ivoire, ambaye anachukua nafasi ya Rais wa Benki hiyo aliyemaliza muda wake, Dkt. Akinumwi Adesina.

Dkt. Tah, Waziri wa zamani wa Fedha wa Mauritania, ameshinda kwa wastani wa asilimia 76.18 ya kura zote zilizopigwa, raundi ya tatu ya mchuano huo.

Alikuwa akiwania nafasi hiyo na wagombea wengine wanne akiwemo Bw. Amadou Hott (Senegal), Samuel Maimbo (Zambia) Abbas Mahamat Tolli (Chad) na mwanamke pekee katika kinyang’anyiro hicho, Bi. Bajabulile Swazi Tshabalala kutoka Afrika Kusini.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ilianzishwa mnamo mwaka 1964 na mwaka huu ikiwa imetimiza umri wa mtu mzima wa miaka 60, ikiwa na wanachama 81, zikiwemo nchi 54 za Afrika.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *