Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameshiriki mechi ya hisani ya kurudisha kwa jamii iliyoandaliwa na Mwamnyeto Foundation, iliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Mechi hiyo ya kirafiki iliyowakutanisha Timu Mwamnyeto dhidi ya Dodoma Combine, imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo, viongozi wa Serikali, wanamichezo maarufu pamoja na mamia ya wakazi wa Dodoma waliojitokeza kuunga mkono juhudi hizo za kijamii.
Lengo la mechi hiyo ni kuchangisha rasilimali kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanywa na Mwamnyeto Foundation, ikiwemo kuwasaidia watoto yatima, wagonjwa, na wenye uhitaji mbalimbali.