DONDOO ZA ALIYOYAZUNGUMZA
▪️Kila mtumishi wa umma ajikite katika kutatua changamoto za watanzania
▪️Kila mtanzania anaowajibu wa kuipenda Tanzania, tusiyumbishwe na watu wasiotutakia mema, Tanzania ni ya Watanzania tuijenge na tuilinde nchi yetu.
▪️Akitokea mtu anakwambia uharibu mali ya umma, huyo anania ya kuihujumu Tanzania, wakatalieni. Wao, watoto zao na ndugu zao hawaishi hapa Tanzania ila wanafanyia biashara maisha ya Watanzania.
▪️Rais Dkt. Samia alishatoa msamaha kwa vijana walioshiriki kwenye tukio lile bila kutambua wanachofanya, hatutarajii watarudia.
▪️Tanzania ni mwalimu wa masuala ya amani na usuluhisi.
▪️Tusiruhusu uhalifu utawale kwenye nchi yetu, tupo kwenye vita ya kiuchumi, wanamezea mate rasilimali zetu, Tanzania tumegundua madini adhimu na tutakuwa nchi 1 Afrika na ya 9 duniani kuwa na madini haya.
