Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza kuanza mara moja kwa utekelezaji wa miradi ya barabara za Nyololo – Igowole – Mtwango na ile ya Mafinga hadi Mgololo ili maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yatekelezwe kwa haraka.
 
Dkt. Mwigulu amemwelekeza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa ahakikishe mkandarasi anapatikana ndani ya wiki mbili na wampatie majibu kuwa kazi hiyo imeshakamilika. “Mkuu wa Mkoa wewe ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara, kwa hiyo simamia suala hilo. Ndani ya wiki mbili mkandarasi apatikane, ahadi ya Mheshimiwa Rais ianze kutekelezwa,” amesema.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Mei 2, 2026) alipozungumza na wakazi wa Igowole, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Igowelo.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *