
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, leo Mei 29, 2026, amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi, katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Bw. Sabi aliambatana na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Bw. Elvis Ndunguru, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Bw. Godwin Semunyu, pamoja na Meneja Mwandamizi wa Mahusiano ya Serikali na Sekta ya Umma, Bw. Azza Mzava.