b8a38551-12b4-4be6-a7b6-84ae2f194b23
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumamosi, Juni 27, 2026 amewasili mkoani Singida kuendelea na ziara yake ya kikazi, ambapo atahutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Msingi Puma, wilayani Ikungi, ataweka jiwe la msingi la jengo la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Tawi la Singida, na baadaye atahutubia mkutano mwingine wa hadhara katika Uwanja wa Maonesho wa Sabasaba, Mandewa.