Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Julai 17, 2026 amekagua na kupokea taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika Julai 25, 2026 katika Viwanja vya Mashujaa, Mtumba, jijini Dodoma.

Katika ukaguzi huo, Waziri Mkuu ameridhishwa na hatua zilizofikiwa na kuwataka wote wanaohusika kuendelea kukamilisha maandalizi yaliyobaki kwa wakati ili maadhimisho hayo yafanyike kwa utaratibu na hadhi inayostahili.

Maadhimisho hayo yataongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *