339484ad-ee9b-4ce2-beed-3f76ff7f42b6 2a95b772-7c49-4ad8-a16e-47063c1edd14Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Afrika inapaswa kutumia mabadiliko yanayoendelea katika siasa, uchumi na usalama duniani kama fursa ya kuharakisha maendeleo yake.
Amesema inapaswa kufanya hivyo kwa kuimarisha uongozi wa kimkakati, kuongeza thamani ya rasilimali zake na kujenga taasisi imara zitakazolinda maslahi ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya Bara la Afrika.
“Afrika isiendelee kuwa uwanja wa ushindani wa mataifa makubwa. Tunapaswa kutumia nafasi yetu ya kimkakati, rasilimali tulizonazo na nguvu ya watu wetu kujiletea maendeleo yenye manufaa kwa wananchi wetu,” amesema.
Waziri Mkuu alisema hayo leo (Jumanne, Julai 21, 2026) alipokuwa Mzungumzaji Mkuu katika Mkutano wa Pili wa Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (National Defence College – Tanzania) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.