Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumapili, Oktoba 11, 2026 ameshiriki ibada katika Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Paulo, jijini London, Uingereza. Ibada hiyo imeongozwa na Kasisi Paula Hollingsworth.

Mara baada ya kuwasili kanisani hapo, Waziri Mkuu alipokelewa na Mshauri wa Askofu (Canon Chancellor), Dkt. Paula Gooder ambaye pia ni Mdhamini wa Kanisa Kuu na anaongoza programu za elimu na mafunzo ya kitheolojia.

Katika Ibada hiyo, Waziri Mkuu aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *