776bc576-447c-48c7-bb48-e37ffd155f74
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewakaribisha wawekezaji kutumia fursa zilizopo Tanzania katika uzalishaji na usindikaji wa mazao, umwagiliaji, pembejeo, uhifadhi, mifugo na uvuvi.
Akihutubia Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue), jijini Des Moines, Marekani, Oktoba 22, 2026, amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri na nishati ili kuwezesha uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko.