WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 14, 2026, amezindua jengo jipya la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, lililopo Kidegembye, mkoani Njombe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Halmashauri, ujenzi wa jengo hilo umegharimu shilingi bilioni 3.8, huku shilingi milioni 300 zikitolewa kwa ajili ya ununuzi wa samani.

Dkt. Mwigulu amesema katika kipindi cha miaka minne hadi mitano, Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga zaidi ya majengo 150 ya aina hiyo, zikiwemo ofisi katika baadhi ya halmashauri kongwe zilizokuwa zikikabiliwa na changamoto ya majengo ya utawala.

Jengo hilo linajumuisha ofisi za Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti wa Halmashauri na wakuu wa idara. Pia lina mifumo ya mawasiliano, usalama na huduma nyingine za kiutendaji kwa ajili ya kurahisisha shughuli za Halmashauri na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Share Story

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *