WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Mei 1, 2026 amewasili mkoani Njombe kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi).
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni : _“Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050”_
