_▪️Wajadili mipango endelevu ya ujenzi wa miundombinu_
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya kikao kazi na wabunge wa mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI pamoja na Wizara ya Fedha.
Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili maendeleo ya miradi ya kimkakati ya miundo




mbinu katika mikoa hiyo hususan ukamilishaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza pamoja na viwanja vya ndege vya Serengeti na Musoma.
Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Spika, Bungeni jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 15, 2026, pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na wakuu wa taasisi za usafirishaji na miundombinu ikiwemo reli, barabara na viwanja vya ndege pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini.