da709151-4856-4981-9bd2-a855dba08fa1
Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba amewaagiza watumishi mbalimbali Nchini wakiwemo waganga wakuu wa Hospitali zote Kuhakikisha kwamba wanathamini utu wa mtu katika kumpatia matibabu kwanza kabla ya kufikiria fedha.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati aliposhiriki kikao cha majumuisho ya ziara zake alizozifanya Mkoani Iringa hivi karibuni.
Sambamba na hilo Waziri Mkuu amedhihirisha maneno hayo kwa vitendo kwa kumpatia tabasamu Bi.Mnyeke mwana mama ambaye alimuomba Waziri Mkuu amsaidie kiti mwendo cha kumsaidia katika shughuli zake.
*Tazama kipande hiki cha Video*